UFADHILI WA MASOMO NCHINI CHINA MWAKA 2015

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA KWA UMMA

UFADHILI WA MASOMO NCHINI CHINA.

Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuwataarifu watanzania wenye vigezo vya kuomba nafasi za masomo ya shahada ya juu ya Uzamili (Postgratuate) katika fani ya gesi na mafuta katika Chuo Kikuu cha Jiosayansi cha China kijulikanacho kama China University of Geosciences (Wuhan), Chini ya ufadhili wa Serikali ya Watu wa China, kuwa muda wa kutuma maombi hayo umeongezwa hadi kufikia tarehe 30/03/2015.

Wizara ya Nishati na Madini inaendelea kuwasisitiza watanzania wenye vigezo kutumia fursa hii kwa kujaza fomu zinazopatikana katika tovuti za http://www.csc.edu.cn/laihuaau www.campuschina.org na www.mem.go.tz. Pia wanaweza kufika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, ghorofa ya Tatu ili kupata taarifa husika.

IMETOLEWA NA;

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

20 Machi, 2015

Powered by Jobs Tanzania