NAFASI ZA KAZI Halmashauri ya Wilaya ya Momba – 3/31/2015

MKURUGENZI MTENDAJI WA WILAYA YA MOMBA ANATANGAZANAFASI YAAJIRA YA WATENDAJI WA VIJIJI

1.Mtendaji Wa Kijiji III- TGS. B NAFASI (2)

A. SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato Sita (VI) na aliyehitimu mafunzo ya AstashahadaiCheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala wa Umma, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
B. KAZI NA WAJIBU WA AFISA MTENDAJI
WAKIJIJI
i.Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika kupanga mipango ya maendeleo na utekelezaji wa mipango;
ii. Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya Kijiji;
iii. Atakuwa Mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji;
iv. Ataratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;
v.Atakuwa Katibu wa Serikali ya Kijiji;
vi. Atatafsiri sera, taratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo za Serikali ya Kijiji;
vii. Ataratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halmashauri ya Kijiji na baadaye kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji na Kata;
viii. Ataratibu vikao vya maendeleo ya Kijiji vitakavyowahusisha wananchi na wataalam waliopo kwenye en eo lake;
ix. Atasaidia katika mikakati mbalimbali
x.Atasimamia na kuratibu matumizi bora ya nguvu kazi;
xi. Atakuwa Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika Kijiji;
xii.Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, Wataalam mbalimbali na
NGO zilizopo katika Kijiji.

C. MASHARTI VA JUMLA KWA WAOMBAJI
i. Awe raia wa Tanzania.
ii. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
iii. Mwombaji aambatishe cheti cha kuzaliwa
iv, Mwombaji aambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV)
v.Maombi yaambatane na vyeti vya kitaaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne au sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
vi. “Testimonials, Provisional results, Statements of results, Hati ya matokeo za kidato cha nne na sita havitakubaliwa”.
vii. Mwombaji kazi ambaye tayari ni mwajiriwa asiombe.
viii. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi mhusika atachukuliwa hatu za kisheria.
ix. Uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi ya Mkurugenzi hauruhusiwi.
x.Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/04/2015

APPLICATION INSTRUCTIONS:

Maombi yatumwe kwa njia ya Posta kupitia
anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
S.L.B 273
TUNDUMA
MOMBA – MBEYA

Powered by Jobs Tanzania