Jobs at Dangote Industries Tanzania

Life at Dangote

At Dangote, our people are key to maintaining and sustaining our vision of touching lives by providing their basic needs. We are committed to maintaining our competitive advantage and so we employ the best talents.

Our Values

Customer Service: As a world-class organisation, we understand that we exist to serve and satisfy our customers. Accordingly, our customer orientation reflects intimacy, integrity and learning.

Entrepreneurship: We continuously seek and develop new business, employing state-of-the-art methods to retain our market leadership.

Excellence: We are a large organisation, working together to deliver the best products and services to our valuable customers and stakeholders. To achieve this, we demonstrate teamwork, respect and meritocracy.

Leadership: We thrive on being leaders in our business, markets and communities. To drive this, we focus on continuous improvement, partnership and professionalism.

MORE AND APPLY 

Powered by Jobs Tanzania

TANGAZO LA KAZI WIZARA YA ELIMU – MARCH 2017


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY
EMPLOYMENT OPPORTUNITIES

The Ministry of Education, Science and Technology is here to announce the Employment opportunities to Mathematics and Science teachers (Diploma and Degree holders). Click HERE to read the announcement in Swahili language. Please share this information to friends as much as you can.


Source: The Ministry Of Eduaction Official Website

Powered by Jobs Tanzania

NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SAYANSI NA HISABATI


NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SAYANSI NA HISABATI WALIOHITIMU MWAKA 2014/2015 KURUDI NYUMA.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia wahitimu wote wa Stashahada na Shahada ya Ualimu katika masomo ya Sayansi na Hisabati wa mwaka 2014/ 15 na miaka ya nyuma, kuwa bado kuna nafasi za ajira, hivyo, wenye sifa watume maombi yao.
Wahitimu walioomba wakati Wizara ilipotangaza nafasi za ajira mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 wasiombe tena kwa kuwa mchakato wa ajira kwa wale wenye sifa unaendelea. Wahitimu walioajiriwa Serikalini wasiombe.
Nyaraka zinazotakiwa kuwasilishwa ni hizi zifuatazo:-
 • Elimu ya sekondari (Kidato cha Nne na Sita);
 • Taaluma ya Ualimu (Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu -PGDE);
 • ‘Academic Trascript’ ya Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu-PGDE);
 • Cheti cha Kuzaliwa;
 • Wasifu (CV) unaoonesha majina matatu. Mwombaji ambaye vyeti vyake vya Elimu na Taaluma havina jina la tatu, akamilishe taratibu za kisheria za kuongeza jina la tatu na kuwasilisha kiapo stahiki pamoja na maombi yake.
UTARATIBU WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-
 1. Mwombaji anatakiwa ‘ku-scan’ vyeti/nyaraka halisi – (Kidato cha 4, 6, Stashahada, Stashahada ya Uzamili na Shahada) na siyo kivuli (photocopy) na kuhifadhi katika ‘File’ moja la ‘pdf’. File lipewe majina matatu ya mwombaji kuanzia la kwanza, kati na la mwisho ndipo litumwe.
 2. Mwombaji atumie anuani ya barua pepe yake mwenyewe na siyo ya mtu mwingine kutuma nyaraka zake.
TANBIHI:
 1. Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 30 Machi, 2017.
 2. Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji zitumwe mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu.
 3. Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika ajira.
 4. Wahitimu ambao waliomba awali mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 na nyaraka zao ziliwasilishwa kikamilifu na kupokelewa, majina yao yamewekwa kwenye tovuti ya Wizara www.moe.go.tz. Hao wasiwasilishe nyaraka hizo tena.
 5. Tangazo hili haliwahusu wahitimu waliofaulu mtihani mwaka wa masomo 2015/16 baada ya kurudia masomo waliyoshindwa mwaka 2014/15.
 6. Nyaraka zote ziwasilishwe kwa barua pepe ifuatayo: apa@moe.go.tz
IMETOLEWA NA
Tarish M.K.
KATIBU MKUU

Powered by Jobs Tanzania