AJIRA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA – 3/24/2015

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela anawatangazia nafasi za kazi za kada ya Madereva. Hivyo waombaji wenye sifa wanatakiwa kutuma maombi ya nafasi hizo za kazi

Dereva Daraja II (x 6)

Ngazi ya Mshahara TGOS A

SIFA ZA KUAJIRIWA
i. Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani kidato cha nne (IV),
ii. Wenye leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na usoefu wa kuendeshea magari kwa mda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali
iii. Wenye Cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II

KAZI ZA KUFANYA

i. Kuendesha magari ya abiria na Malori

ii. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari kugundua ubovu unaohitaji matengenezo madogomadogo katika gari
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari
iv. Kutuma na kuandika daftari la safari “Log – Book” kwa safari zote

SIFA ZA JUMLA
Muombaji ni lazima awe raia wa Raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45, muombojai ni lazima aambatanishe cheti cha kuzaliwa, vyeti vya ujuzi, vyeti vya taaluma na wasifu wake. Barua za mombi ya kazi ziandikwe kwa mkono

APPLICATION INSTRUCTIONS:

Mwisho wa kupokea maombi hayo ya kazi ni tarehe 03/04/2015. Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa kutumia anuani ifuatayo

MKURUGENZI WA MANISPAA

S.L.P 735

ILEMELA

IMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILEMELA

JOHN PAUL WANGA
MKURUGENZI WA MANISPAA
ILEMELA

Powered by Jobs Tanzania